Soka: Werder Bremen juu kileleni.
10 Desemba 2006Matangazo
Mlinzi kutoka Brazil Naldo ameweka wavuni mabao matatu wakati Werder Bremen ikirejea kileleni katika ligi ya Ujerumani Bundesliga, baada ya kutolewa katika kinyang’anyiro cha kombe la ligi ya mabingwa , Champions League, na kuikung’uta Eintracht Frankfurt kwa mabao 6-2.
Ushindi huo mjini Frankfurt umeifikisha Bremen katika point 33, point mbili zaidi ya VFB Stuttgart ambao walipata ushindi mwembamba wa bao 1-0 dhidi ya Buchum, wakati mabingwa watetezi Bayern Munich walipata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Ernegie Cottbus