SOKOTO: Hofu ghasia kuzuka kaskazini ya Nigeria
19 Julai 2007Matangazo
Shehe wa Kisunni wa itikadi kali ameuawa baada ya kupigwa risasi na nje ya msikiti katika mji wa Sokoto,kaskazini mwa Nigeria.Haijulikani nani aliehusika na mauaji hayo,lakini Waislamu wa madhehebu ya Kisunni mjini Sokoto wanasema, wanawashuku wanachama wa kundi hasimu la Kishia. Kwa mujibu wa mashahidi,polisi na wanajeshi wamesambazwa katika mji huo kuzuia machafuko. Miaka miwili iliyopita,mji wa Sokoto ambao ni kituo kikuu cha Waislamu nchini Nigeria, ulishuhudia mapambano makali kati ya Washia na Wasunni waliokuwa wakigombea haki pekee ya kusali katika msikiti mkuu wa mji huo.Si chini ya watu 10 waliuawa katika machafuko hayo.