Hifadhi ya Taifa ya Virunga imetangaza kwamba Sokwe wa milimani anayeitwa Mafuko amezaa mapacha wawili wa kiume katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, eneo ambalo limekumbwa na vita.
Sokwe wa kike wa mlimani Mafuko akiwa na mapacha wake wachangaPicha: Virunga National Park/REUTERS
Matangazo
Hifadhi ya Taifa ya Virunga imetangaza kwamba Sokwe wa milimani anayeitwa Mafuko amezaa mapacha wawili wa kiume katika eneo la mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, eneo ambalo limekuwa likikumbwa na vita kwa muda mrefu.
Tukio hili limeelezwa kama hatua muhimu sana katika juhudi za uhifadhi wa aina hii adimu ya sokwe.
Mapacha hao wawili wa kiume walizaliwa na Sokwe Mafuko, na waligunduliwa tarehe Januari 3, 2026 na kulingana na taarifa ya hifadhi hiyo, mapacha hao walionekana kuwa na afya nzuri wakati walipoonekana kwa mara ya kwanza.
Virunga, iliyo na zaidi ya maili za mraba 3,000, ni hifadhi kongwe zaidi barani Afrika na ni makazi ya Sokwe wa milimani waliobaki duniani.
Mbuga ya wanyama ya Virunga ni pepo ndogo iliyopo mashariki mwa Kongo. Ajabu ni kwamba kampuni moja ilitaka kuchimba mafuta katika mbuga hiyo. Wasiwasi huo umetoweka kwa sasa, lakini mbuga hiyo ina maadui wengine.
Mazingira bado kama ni Pepo
Ni hali ya ahueni katika hifadhi hii kongwe ya Afrika. Mbuga ya wanyama ya Virunga kwa sasa imeepushwa na uchimbaji wa mafuta uliyokuwa ufanywe na kampuni ya Uingereza ya Soco International. Hayo ni mafanikio ya wakfu wa kutetea mazingira wa WWF. Wakfu huo ulipeleka malalamiko katika shirika la ushirikiano na maendeleo ya kiuchumi OECD.
Picha: WWF/Brent Stirton
Utunzaji wa mazingira wenye historia ndefu
Hapa ndipo mahala ambapo mashine za uchimbaji mafuta zingechimba mita kadhaa chini ya ziwa Edward, lililoko katika mbuga ya taifa ya Virunga kwenye mpaka wa Uganda. Tangu mwaka 1925 wakoloni wa Kongo Ubelgiji, walilitangaza eneo hili lenye volkano hai, misitu ya tropiki na milima ya theluji kuwa hifadhi ya asili. Na mwaka 1976 UNESCO iliitambua mbuga hiyo kuwa turaathi ya Dunia.
Picha: WWF/Brent Stirton
Hofu ya uwezekano wa mafuta kumuagika
Kama hapa katika kijiji cha Kavanyongi zinaishi Karibu familia 50,000 kwa kulitegemea ziwa Edward: Ziwa hili linawapatia maji safi ya kunywa na pia maji ya kupikia. Uvuvi ni chanzo muhimu cha chakula na mapato kwa wakaazi wa eneo hili. Wengi walihofia kwamba uchimbaji uliyokuwa umepangwa ungechafua ziwa lao.
Picha: WWF/Brent Stirton
Maisha mapya
Katika soko la Kila wiki la Vitshumbi kwenye mwambao wa kusini mwa ziwa Edward, wanawake kutoka vijiji vya jirani huuza samaki wakavu. Familia nyingi zilikimbilia hapa kuepuka mapigano baina ya makundi hasimu ya wapiganaji katika maeneo mengine ya Kongo mashariki . Hata mbuga hii yenyewe imekuwa eneo la mapigano makali kwa muda mrefu. Lakini kwa sasa watu hawa wamejenga maisha mapya hapa.
Picha: WWF/Brent Stirton
Makaazi ya sokwe wa milimani
Katika milima ya volkano ya mbuga ya Virunga, wanaishi karibu sokwe 200 wa milimani. Wanyama hao wanaokabiliwa na kitisho cha kutoweka walikuwa sababu muhimu ya eneo hilo kutangazwa kuwa turaathi ya dunia. Lakini majangili wameendelea kuwauwa tena na tena wanyama hao wenye haya. Nyama yao inachukuliwa kuwa chakula kitamu sana na inauzwa bei ghali.
Picha: WWF/Brent Stirton
Misitu hatarini
Mbuga ya taifa ya Virunga ni makaazi ya spishi zaidi ya 700 za ndege na spishi 2,000 tófauti za mimea. Hata hivi viko hatarini kutoweka. Kila mwaka wakaazi hukata maeneo makubwa ya misitu kwa ajili ya kuwauzia kuni wakaazi wa mji wa Goma. Hata wapiganaji hukata misitu kwa ajili ya mkaa ili waweze kufadhili ununuzi wa silaha na risasi.
Picha: WWF/Brent Stirton
Shirikisha raia
"Tunapaswa kuwaonyesha watu kuwa uhifadhi unaweza kuwa na manufaa ya kiuchumi, vinginevyo Virunga haitanusurika," alisema Emmanuel de Morode, Mkurugenzi wa mbuga hiyo tangu miaka mitano iliyopita. Kwa hivyo Mbeligiji huyo anategemea mitambo midogo ya maji kuzalisha umeme au kwa kutumia makaa ya mawe. Mwezi Aprili Merode ambaye ni mpinzani mkubwa wa uchimbaji mafuta alinusurika kuuawa.
Picha: Getty Images
Hakupaswi kuwa na unyonyaji
Mbuga ya Virunga ina uwezo mkubwa. Kwa mujibu wa utafiti uliyofanywa na Wakfu wa WWF, mbuga hii inaweza kutoa hadi nafasi 45,000 za ajira katika maeneo ya kuzalisha umeme wa maji, uvuvi, utalii wa ikolojia, utabibu, utafiti na elimu. Mazingira na biashara vinapaswa kwenda sawia. Kwa mujibu wa WWF, usimamizi endelevu wa mbuga ya Vurunga unaweza kuingiza Karibu euro milioni moja kila mwaka.
Picha: WWF/Brent Stirton
Vizazi vilivyopotea
Kama injini ya kiuchumi, mbuga ya taifa Virunga inaweza kuchangia amani na maendeleo endelevu katika eneo linaloizunguka. Kama ilivyokuwa kabla, eneo la mashariki mwa Kongo ndiyo moja ya maskini zaidi barani Afrika. Kwa miongo kadhaa, maisha ya kila siku yemegubikwa na mapigano baina ya makundi hasimu, na vizazi vya vijana vimekuwa bila fursa za elimu wala ajira katika eneo hilo.
Picha: WWF/Brent Stirton
Makampuni ya mafuta hayajakata tama kabisaa
Mwaka 2011 mafuta yaligunduliwa katika mbuga ya Virunga, na serikali ya Kongo iliingia mkataba wa utafiti na kampuni ya Uingereza ya Soco International. Kampuni hiyo sasa ilikubaliana na WWF kusitisha utafiti huo hadi serikali ya Kongo na UNESCO zithibitishe kuwa shughuli zake hazitaiathiri mbuga hiyo. Hii inamaanisha kuwa mbuga ya Virunga inaendelea kuangaliwa na makampuni ya mafuta.
Picha 101 | 10
Kulingana na hifadhi ya Virunga, suala la kuwahudumia mapacha huwa na changamoto, hasa katika miezi ya mwanzo ambapo watoto hao wa Sokwe hutegemea kikamilifu ungalizi kutoka kwa mama. Kwa sasa, wafanyakazi wa hifadhi wanawafuatilia kwa karibu ili kuhakikisha wanaendelea vyema.
Picha zilizotolewa na hifadhi zinaonyesha mama wa mapacha hao, Mafuko, mwenye umri wa miaka 22, akiwa amewakumbatia watoto wake mapacha, akiwa ameketi chini miongoni mwa matawi yenye majani ya kijani.
Mafuko alizaliwa katika familia ya Kabirizi, lakini alijiunga na familia ya Bageni miaka sita baada ya mama yake kuuawa mwaka 2007 na watu wenye silaha, kulingana na maelezo ya hifadhi ya Virunga.
Hadi sasa Mafuko amezaa Sokwe saba, ikiwemo mapacha waliokufa wiki moja tu baada ya kuzaliwa mwaka 2016. Familia ya Bageni sasa ina jamaa 59, na ndiyo familia kubwa zaidi ya sokwe katika hifadhi hio.