1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Solana: Ulaya haimo vitani.

20 Machi 2004

BRUSSELS:
Mwanadiplomasia mkuu wa UU Javier Solana
ameonya dhidi ya kuchukuliwa tahadhari ya
kupita mpaka kwa sababu ya mashambulio ya
kigaidi mjini Madrid. Ulaya haimo vitani,
mjumbe huyo wa Siasa ya Nje na Usalama ya UU
aliliambia gazeti la Kijerumani BILD AM
SONNTAG. Lazima ugaidi uchukuliwe hatua kali,
lakini nchi hazina haja ya kubadilisha mifumo
yao ya kimaisha na itikadi zao za kidemokrasi,
alisisitiza Bwana Solana. Kufuatana na
mashambulio ya Madrid, Mawaziri wa Mambo ya
Ndani wa UU hapo Ijumaa ya jana waliwafikiana
kumteua mjumbe maalumu wa UU. Mjumbe huyo
atakabidhiwa jukumu la kuwiyanisha harakati za
usalama na mapigano dhidi ya ugaidi ya nchi
zanachama 25 za UU.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW