27 Desemba 2016
Matangazo
Kura ya urais ilipangwa kufanyika tarehe 28 Desemba. Lakini afisa wa tume ya uchaguzi amewaeleza wanahabari kuwa tarehe mpya ya uchaguzi huo itakuwa ni mwishoni mwa mwezi Januari, wakati nchi hiyo itakapowachagua wabunge wenye jukumu la kumchagua rais. Rais nchini Somalia hachaguliwi moja kwa moja kwa kura za wananchi. Wanachama wa upinzani wamekuwa na wasiwasi juu ya kucheleweshwa kwa uchaguzi huo kwa muda mrefu, wakisema mchakato umeathiriwa na udanganyifu unaotaka kukipendelea chama tawala.