1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia yamfukuza mwanadiplomasia wa Ethiopia

Josephat Charo
30 Oktoba 2024

Somalia imeamuru kufukuzwa kwa mwanadiplomasia wa cheo cha juu wa ubalozi wa Ethiopia jana Jumanne katika hatua ya hivi karibuni ya kuzorota kwa mahusiano kati ya nchi hizo jirani za mashariki mwa Afrika.

Uturuki ilijaribu kuzisuluhisha Somalia na Ethiopia
Mzozo kati ya majirani Somalia na Ethiopia unazidi kufukuta.Picha: Arda Kucukkaya/Anadolu/picture alliance

Hali ya wasiwasi imekuwa kubwa tangu Ethiopia ilipofikia makubaliano Januari mwaka huu kujenga bandari katika eneo lililojitenga la Somaliland.

Somalia tayari ilimtimua balozi wa Ethiopia mnamo Aprili mwaka huu na kumrudisha nyumbani balozi wake kutoka mjini Addis Ababa. Siku ya Jumanne wizara yake ya mambo ya nje ilitangaza katika taarifa kwamba inampa Ali Moahamad Adan, saa 72 aondoke Somalia.

Wizara hiyo haikutoa sababu maalum, lakini ilisema Adan hakuheshimu sheria za nchi na kushindwa kujiepusha na masuala ya ndani ya Somalia. Wizara ya mambo ya nje ya Ethiopia haijatoa kauli ya kujibu hatua hiyo ya Somalia.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW