1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
MigogoroSomalia

Somalia yanafanya juhudi kuwaokoa mateka wa Umoja wa Mataifa

11 Januari 2024

Serikali ya Somalia imesema inafanya juhudi kujaribu kuwaokoa abiria wa helikopta ya Umoja wa Mataifa iliyokamatwa na wanamgambo wa itikadi kali wa Al-Shabaab jana Jumatano.

Helikopta ya Umoja wa Mataifa yakamatwa na wanamgambo wa itikadi kali wa Al-Shabaab
Helikopta ya Umoja wa Mataifa yakamatwa na wanamgambo wa itikadi kali wa Al-ShabaabPicha: Gerard Gaudin/Belga/imago images

Helikopta hiyo iliyokodiwa na Umoja wa Mataifa kwenda kutoa msaada wa matibabu ilipata hitilafu na kulazimika kutua karibu na kijiji cha Hindhere katikati mwa Somalia, eneo ambalo linadhibitiwa na wanamgambo wa Al-Shabaab.

Raia wawili wa Somalia na wengine kadhaa wa kigeni walikuwemo ndani ya chombo hicho na wengi wamechukuliwa mateka na wapiganaji hao. Hadi sasa haijafahamiwa idadi kamili ya waliotekwa nyara na iwapo kama wengine waliofanikiwa kutoroka.

Waziri wa habari wa wa Somalia, Daud Aweis amearifu kwamba serikali ya Somalia inafanya jitihada za kuwaokoa watu watu hao. Hata hivyo maafisa wa kijeshi wameashiria itakuwa vigumu kulifikia eneo mkasa ulipotokea.

Kanali Abdullahi Isse, aliye kwenye moja kambi iliyo umbali wa kiasi kilometa 100 kaskazini mwa kijiji cha Hindhere amesema wanajeshi hawana mipango ya kuanzisha operesheni ya uokoaji.

Amesema eneo mkasa ulikotokea linadhibitiwa na Al-Shabaab kwa zaidi ya miaka kumi na hata wakaazi wake wanawaunga mkono wanamgambo hao.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW