1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
Migogoro

Somalia yaomba walinda amani wasiondolewe kwa siku 90

22 Septemba 2023

Somalia inataka mpango wa kuwapunguza walinda amani wa Umoja wa Afrika nchini mwake ucheleweshwe kwa miezi mitatu.

Somalia Tabda
Wanajeshi wa jeshi la Kenya wamesimama katika eneo la shimo kwenye kituo chao cha Tabda, ndani ya Somalia.Picha: Ben Curtis/AP Photo/picture alliance

Kulingana na barua ya serikali ambayo shirika la habari la AFP limepata nakala yake, ombi hilo limetokana na hali ya kushindwa mara kadhaa katika mapambano yake dhidi ya wanamgambo wa Al-Shabaab.

Soma pia: Somalia: Umoja wa Mataifa kuongeza vikosi vya walinda amani

Mshauri wa kitaifa wa masuala ya usalama nchini Somalia aliuandikia Umoja wa Mataifa barua na kuomba awamu ya pili ya uondoaji wa vikosi vya amani isitishwe kwa siku 90. Kulingana na barua hiyo, jumla ya walinda amani 3,000 wa ATMIS, wanatarajiwa kuondoka Somalia ifikapo mwisho wa Septemba kwenye awamu hiyo.

Duru za kidiplomasia zilithibitisha uhalali wa barua hiyo. Hata hivyo maafisa kadhaa wa Somalia walioulizwa, hawajatoa kauli yoyote.MOGADISHU Mripuko wa bomu waua watu wawili mjini Mogadishu, Somalia.

Maazimio ya Umoja wa Mataifa yanataka kikosi cha ATMIS kiondoke Somalia kabisa ifikapo mwishoni mwa mwaka ujao, hivyo kuhamisha kikamilifu usalama kwa jeshi la taifa na polisi.