1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia yapinga vikali kutambuliwa Somaliland

28 Desemba 2025

Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud amesema hatua ya Israel kulitambua jimbo lililojitenga la Somaliland kama taifa huru ni tishio kwa usalama na uthabiti wa dunia.

Somalia-
Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud yapinga vikali kutambuliwa kwa Somaliland kama taifa huru.Picha: Annegret Hilse/REUTERS

Akizungumza katika kikao cha dharura cha Bunge mjini Mogadishu, Mahamud amekosoa tangazo la juzi Ijumaa la Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu akiitaja hatua hiyo kama shambulio la wazi dhidi ya mamlaka, uhuru, umoja wa eneo na watu wa Jamhuri ya Somalia.

Somaliland ilijitangazia uhuru kutoka Somalia mwaka 1991 na kwa miongo kadhaa imekuwa ikitafuta kutambuliwa kimataifa. Ingawa inajiendesha kama jamhuri huru yenye sarafu, pasi na jeshi lake, imeendelea kutengwa kidiplomasia tangu ilipotangaza kujitenga.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW