1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia kusitisha safari za ndege za Ethiopian Airlines

22 Agosti 2024

Mamlaka ya usafiri wa anga ya Somalia imetishia kusimamisha safari zote za shirika la ndege la Ethiopia Airlines kwenda nchini humo, hatua ya hivi karibuni katika mzozo wa muda mrefu kati ya nchi hizo mbili.

Wasafiri wakiabiri ndege ya shirika la ndege la Ethiopia.
Wasafiri wakiabiri ndege ya shirika la ndege la Ethiopia.Picha: Solomon Muchie/DW

Mamlaka hiyo ya usafiri wa anga ya Somalia SCAA imesema shirika la ndege la Ethiopia Airlines, ambalo ni shirika kubwa zaidi la ndege barani Afrika, halijashughulikia malalamiko ya hapo awali ikiwemo kile walichokiita “masuala ya uhuru.”

Mamlaka hiyo imeeleza kuwa, iwapo malalamiko hayo hayatapa ufumbuzi kufikia Agosti 23, basi haitakuwa na budi ila kusimamisha safari zote za ndege za Ethiopian Airlines kwenda Somalia.

Soma pia:Watu 11 wauawa katika shambulizi la kigaidi Mogadishu

Ethiopia ilitia saini makubaliano na jimbo la Somaliland mapema mwaka huu kukodisha kilomita 20 za pwani katika kipindi cha miaka 50, kuiruhusu Ethiopia isiyo na bahari kufikia eneo la pwani.

Kwa upande wake, Somaliland ambayo ilitangaza uhuru wake kwa kujitenga na Somalia mwaka 1991, imesema Ethiopia itakuwa nchi ya kwanza kuitambua rasmi Somaliland kama taifa huru.