Somalia yatoa wito wa kuhitimishwa ujumbe wa UNSOM
10 Mei 2024Somalia imeutaka Umoja wa Mataifa kuhitimisha kazi za ujumbe wake wa kisiasa wa UNSOM ambao umekuwepo nchini humo kwa zaidi ya muongo mmoja, wakati wajibu wake wa sasa utakapofikia mwisho mwezi Oktoba.
Soma pia: Hali ya haki za binadamu Somalia inatia wasiwasi
Ujumbe wa UNSOM ulianzishwa mwaka 2013 na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kuunga mkono mamlaka ya Somalia katika kipindi cha mpito cha kuelekea demokrasia na utawala wa sheria, baada ya zaidi ya miaka 20 ya mzozo baina ya wanamgambo, makundi yenye itikadi kali za Kiislamu na magenge ya kihalifu.
Soma pia: Amnesty: Mashambulizi ya anga ya Somalia yaliwaua raia
Katika barua kwa Baraza la Usalama, ambayo shirika la habari la AFP limeipata, waziri wa mambo ya nje wa Somalia Ahmed Moallim Fiqi, aliomba kusimamishwa kwa mamlaka ya ujumbe huo wa UNSOM, kufuatia kuzingatiwa kwa kina vipaumbele vya kimkakati vya nchi hiyo.