1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Somalia yazipiga marufuku TikTok, Telegram na 1XBet

22 Agosti 2023

Somalia imepiga marufuku mtandao wa kijamii wa TikTok, programu ya kutuma ujumbe ya Telegram na tovuti ya kamari ya mtandaoni ya 1XBet.

Wanachama wa kundi la al Shabaab huchapisha habari na shughuli zao kwenye TikTok na Telegraph.
Wanachama wa kundi la al Shabaab huchapisha habari na shughuli zao kwenye TikTok na Telegraph.Picha: Joly Victor/abaca/picture alliance

Waziri wa mawasiliano wa Somalia, Jama Hassan Khalif, amesema hatua hiyo inalenga kuzuia kuenea kwa maudhui yasiyofaa na propaganda kwa jamii nchini Somalia.

Waziri huyo wa mawasiliano ameziagiza kampuni za mitandao kuacha kuitangaza mitandao iliyopigwa marufuku ambayo magaidi na makundi ya watu wasio na maadili huitumia kueneza picha chafu na taarifa potofu kwa umma.

Uamuzi huo umetolewa siku chache baada ya Rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud kusema mashambulizi ya kijeshi dhidi ya al Shabaab yanalenga kuliondoa kundi hilo lenye uhusiano na kundi la kigaidi la al Qaeda katika muda wa miezi mitano ijayo.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW