Somalia
24 Januari 2009Matangazo
Mogadishu:
Raia wasiopungua 14 wameuwawa hii leo mjini Mogadischu,mtu mmoja alipojiripua akiwa ndani ya gari karibu na kituo cha kikosi cha kulinda amani cha Umoja wa Afrika nchini Somalia-Amisom.Naibu diwani wa mji mkuu wa Somalia Mogadishu,Abdifatah Ibrahim Shaweye ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP mtu huyo aliyeyatolea mhanga maisha yake amepita kwa nguvu na kujiripua karibu na basi la abiria katika njia panda ya K4,kusini mwa Mogadischu.Maabiria wote 14 na gaidi wameuwawa.