Somaliland yafanya uchaguzi
13 Novemba 2017Matangazo
Jimbo hilo ambalo zamani lilikuwa koloni la Waingereza lilijipatia uhuru wake mwaka 1960 lakini siku kadhaa badae likajiunga na Somalia na kuwa nchi moja ingawa mwaka 1991 baada ya miaka kadhaa ya mivutano mikubwa na serikali kuu mjini Mogadishu, Somaliland ikajitangazia uhuru na kujitenga Somalia.Uhuru huo lakini hautambuliwi kimataifa. DW imezungumza na mchambuzi wa kisiasa Ahmed Rajab kuhusu uchaguzi huo na kwanza anaeleza ni mambo gani hasa yanayoifanya Somaliland kuwa tafauti na Somalia hasa kwenye suala la kufanya uchaguzi kwa njia ya amani na ya kidemokrasia.