1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sommer aiacha Uswisi kwa ajili ya kuzaliwa kwa mtoto wake

17 Juni 2021

Mlinda lango wa timu ya taifa ya Uswisi Yann Sommer, amesafiri kuelekea Ujerumani kujiunga na mkewe wakati wa kujifungua. Sommer amekiacha kikosi cha timu ya taifa ya Uswisi katika michuano ya EURO 2020.

Fußball Bundesliga FC Bayern - Mönchengladbach
Picha: Getty Images/AFP/C. Stache

Mlinda lango wa timu ya taifa ya Uswisi Yann Sommer amekiacha kikosi cha timu hiyo ili kujiunga na mkewe wakati anajifungua mtoto wao wa pili. Soma Lijue kundi A la michuano ya Euro 2020.

Shirikisho la Soka la Uswisi limesema Sommer amesafiri kuelekea Ujerumani baada ya kufungwa 3-0 na Italy hapo jana Jumatano huko Roma.

Yann SommerPicha: Reuters/G. Fuentes

Haijulikana iwapo Sommer atarudi wakati wa mechi ya mwisho ya kundi A mnamo Jumapili dhidi ya Uturuki itakayochezwa mjini Baku. Uswisi inahitaji ushindi katika mechi hiyo ili kufuzu kwa raundi ya 16 bora.

Sommer anaichezea timu ya Ujerumani Borussia Moenchengladbach. Mnamo Aprili mlinda mlango huyo aliandika katika akaunti yake ya Instagram kuwa mke wake anatarajia kujifungua mtoto wa kike. Tayari wanamtoto mwengine wa kike.

APE

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW