1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sonko aanza tena mgomo wa kula

18 Oktoba 2023

Kiongozi wa upinzani wa Senegal anayetumikia kifungo gerezani Ousmane Sonko anasema ameanza tena mgomo wa kula aliousitisha mwezi uliopita kuelekea uchaguzi mwakani.

Senegal Oppositionsführer Ousmane Sonko
Kiongozi wa upinzani wa Senegal, Ousmane Sonko.Picha: Seyllou/AFP

Sonko alitupwa jela mwezi Julai mwaka huu alipotiwa hatiani kwa makosa ya kuchochea fujo, kushiriki vitendo vya uhalifu na kundi la kigaidi na kuvuruga usalama wa dola kuhusu matukio ya mwaka 2021.

Sonko, mwenye umri wa miaka 49, amemtuhumu rais wa Senegal Macky Sall kwa kujaribu kumzuia asigombee katika uchaguzi wa rais, madai ambayo Sall anayakanusha. 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW