SiasaSenegal
Sonko aigomea serikali mpya ya Faye
2 Juni 2026
Matangazo
Tangazo la jana la Faye linakuja ikiwa ni takribani wiki mbili tangu amfukuze kazi Sonko, na kulivunja baraza lake la mawaziri kwa kutafautiana juu ya uendeshaji uchumi.
Sonko, ambaye ni mashuhuri zaidi kuliko Faye, alichaguliwa hapo hapo kuwa spika wa bunge na wafuasi wake katika hatua inayoashiria mkwamo mpya wa kisiasa ndani ya taifa hilo la magharibi ya Afrika.
Sonko ndiye kiongozi mkuu wa Pastef, chama alichokianzisha mwaka 2014 na ambacho Faye ni mwanachama wake na kinachohodhi viti 130 kati ya 165 bungeni.
Hapo jana, waziri mkuu mpya, mchumi Ahmadou Al Aminou Mohamed Lo, alitangaza majina ya mawaziri wapya 30, lakini Sonko alisema chama chake hakitajiunga na serikali hiyo.