Sonko asema mapinduzi ya Guinea Bissau sio halali
28 Novemba 2025
Matangazo
Akijibu maswali kutoka kwa wabunge, Sonko amesema tume ya uchaguzi nchini Guinea Bissau lazima iweze kumtangaza mshindi.
Hapo jana baada ya jeshi kumuapisha Jenerali Horta Nta Na Man kama rais wa mpito atakaeshikilia wadhifa huo kwa kipindi cha mwaka mmoja, kiongozi huyo alisema mapinduzi hayo yalihitajika ili kuzuia njama ya walanguzi wa dawa za kulevya kudhibiti demokrasia ya nchi hiyo na akaapa kusimamia kipindi hicho cha mpito kilichoanza mara moja.
Umoja wa Ulaya na mwenyekiti wa Umoja wa Afrika Mahmoud Ali Youssouf pia wametoa wito wa kurejeshwa kwa utaratibu wa kikatiba.