Southgate kumaliza kipindi cha mpito
14 Novemba 2016Mchezo huo katika uwanja wa Wembley utakuwa wa nne na wa mwisho kwa kipindi cha mpito cha Southgate na kufuatia ushindi wa mabao 3-0 siku ya Ijumaa dhidi ya Scotland katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia , anatarajiwa kukabidhiwa jukumu kamili la kuifunza timu hiyo ya taifa ya England.
Kama alivyo Southgate , Lopetegui amepata kuaminika na chama cha kandanda nchini Uhispania kwa kuwa kocha bora katika timu ya vijana chini ya miaka 21, wakati mchezo wa kujiamini wa kupasiana mpira wa Uhispania ni kitu ambacho Southgate anataka England iufuate.
Kocha wa Marekani Jergen Klinsmann ameitaka timu yake kukusanya hisia za hasira wakati wanajaribu kurejea katika hali ya kawaida kutoka katika kipigo dhidi ya Mexico katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza katika fainali za kombe la dunia dhidi ya Costa Rica kesho Jumane (15.11.2016).
Kikosi cha kocha Klinsmann kilipata pigo kubwa dhidi ya Mexico siku ya Ijumaa, wakati Rafa Marquez alipofunga katika dakika ya 89 bao muhimu katika ushindi wa mabao 2-1 katika uwanja wa Mapfre.
Kipigo hicho kilikuwa ni janga kubwa kwa Marekani katika duru ya ufunguzi wa mchezo wa kufuzu kucheza katika fainali za kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi katika kanda ya CONCACAF.
Wakati kumebakia pointi nyingi za kuwania katika duru ya timu sita, Marekani inahaha kuzuwia kupoteza michezo zaidi na kukimbiwa na Mexico na Costa Rica , mahasimu wao wakubwa katika kupata nafasi za moja kwa moja za kufuzu kucheza fainali za kombe la dunia.
Timu tatu zitakazomaliza juu ya msimamo wa kundi hilo, zinafuzu moja kwa moja kuingia katika fainali za dunia wakati timu ya nne inaingia katika mchezo wa mchujo.
Na huko mashariki ya mbali, kocha Marcello Lipi amesema China inahitaji kuondokana na fikira za kuwa wanyonge wakati watakapopambana katika mchezo mgumu wa kwanza akiwa kama kocha wa timu hiyo, mchezo wa kufuzu kucheza katika fainali za kombe la dunia dhidi ya Qatar, mchezo ambao kila timu haithubutu kushindwa.
Wakati Lippi , ambaye aliifunza Italia na kushinda kombe la dunia mwaka 2006, anakiri kwamba China iliyoko chini kabisa ya msimamo wa kundi la mataifa ya kanda hiyo inahitaji maajabu iwapo inataka kufika katika fainali za kombe la dunia mwaka 2018, amesema umihimu kwake ni kurejesha imani.
"Ni muhimu kurejesha imani ya timu," amesema Lippi , kwa mujibu wa tovuti ya FIFA, kabla ya pambano la kesho Jumanne mjini Kunming.
Mhariri: Yusuf Samu