SRINAGAR. Waasi walipua gruneti
5 Septemba 2005Matangazo
Waasi wasiopendelea mageuzi nchini India wamerusha gruneti katika barabara yenye shughuli nyingi katika mji wa Kashmir na kuwajeruhi watu kadhaa masaa machache kabla ya mkutano baina ya waziri mkuu wa India na wawakilishi wanaotaka kujitenga katika jimbo la Kashmir.
Shambulio hilo limetokea katika mji wa Shopian kusini mwa Srinagar.
Hakuna kikundi chochote kilichodai kuhusika na shambulio hilo lililolenga msafara wa kijeshi na badala yake kulipuka barabarani.
Waziri mkuu wa India Manmohan Singh kwa mara ya kwanza tangu serikali mseto ichukue mamlakna nchini India atafanya mazungumzo na wanaharakati hao wanaotaka kujitenga jimbo la Kashmir.