ST PETERSBURG:Rais Vladmir Putin wa Urussi ailaumu Israel kwa kuwa na malengo tofauti katika opresheni ya kijeshi Lebanon
16 Julai 2006Matangazo
Mkutano wa viongozi wa nchi tajiri kiviwanda duniani G8 unaofanyika mjini St Petersburg Urussi umegubikwa na suala la mzozo wa mashariki ya kati.
Rais wa Urussi Vladmir Putin ameilaumu Israel kwa kuwa na malengo mengine ya kijeshi badala ya kulenga kuwakomboa wanajeshi wake wawili waliotekwa nyara na wanamgambo wa Hezbollah.
Amesema opresheni za kijeshi za Israel lazima ziwe na usawa.
Kwa upande wake rais Bush wa Marekani ameitaka Syria kukomesha mashambulio ya wanamgambo wa Hezbollah dhidi ya Israel.
Rais Bush na Putin walifanya mkutano wao ambapo walizungumzia masuala ya mgogoro wa Nuklia wa Iran na Korea Kaskazini lakini viongozi hao hawakukubaliana juu ya Urussi kujiunga na shirika la biashara duniani WTO.