1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

STADI WA GHANA MICHAEL ESSIEN KUUZWA KWA EURO Mil.45:

18 Julai 2005

Rais wa klabu ya Ufarabnsa ya olimpik Lyon,Jean-Michel Aulas, anadai kwamba, ikiwa klabu bingwa ya Uingereza Chelsea,inamtaka stadi wa Ghana Michal Essien,itapaswa ilipe kitita cha Euro milioni 45 kumkomboa.

Aulas ambae hapo kabla alidai Essien hauzwi, amebadili nia alipozungumza na gazeti mashuhuri la dimba la Ufarabnsa L’Equipe hivi ileo.

Alisema kwamba, chelsea iliridhia dai la Liverpool la kitita cha Euro milioni 15 kumnunua Steven Gerrard.Na kwahivyo, Essien ataihama Lyon tu kwa kitita kama hicho-alisema rais wa Lyon.

Olympique Lyon wakati huu wako Korea Kusini wakiania Kombe la amani-Peace Cup ikiwa sehemu ya maandalio yao ya msimu mpya.Essien amefuatana na timu yake huko Asia na mkataba wake na Lyon unadumu hadi 2008.Ameonesha hamu kuu lakini ya kujiunga na Chelsea.

Katika dimba la kirafiki,Chelsea jana iliizaba Benefica Lisbon ya Ureno bao 1-0 mjini Lisbon.Wakati Lyon iklo Asia, Chelsea inafunga safari ya Marekani ikipanga mechi 2-moja na AC Milan ya Itali.Chelsea itaanza kutetea taji lake la ubingwa wa Premier League kuanzia August,14.

Katika kinyan’ganyiro cha Kombe la GOLD CUP la shirikisho la CONCACAF,Colombia imekata jana tiketi yake ya nusu-finali kwa kuizaba mabingwa watetezi Mexico mabao 2:1.Colombia sasa itakutana na panama kuania nafasi ya finali ya kombe hili linalochezwa kila baada ya miaka 2.Panama ilipiga kumbo Africa Kusini kwa mabao 5-3 kupitia changamoto ya mikwaju ya penalty.Afrika kusini ilikuwa suluhu bao 1:1 na Panama hadi dakika ya mwisho ya 90.Katika nusu finali ya pili,Marekani imechukua nafasi hiyo kwa kuitoa hapo jumamosi jamaica kwa mabao 3:1.Marekani ina miadi sasa na Hondurus.

Barani Africa,Raja Casablanca ya Morocco,imelitwaa Kombe la kiti cha Ufalme (THRONE CUP) mwishoni mwa wiki .Kama Panama katika CONCACAF,Raja nayo ilihitaji changamoto za mikwaju ya penalty kuipiga kumbo Olympique Khouribga kwa mabao 5-4.Hili ni taji la 6 la Raja.

Nje ya medani ya riadha, wananchi wengi wa New Zealand wangependelea kuona seriali yao inaizuwia timu yao ya Cricket kutembelea Zimbabwe mwezi ujao-hii ni kwa muujibu ya maoni ya wananchi yaliochapishwa leo.

NZ inaongoza mgomo wa kususiwa Zimbabwe kutokana na tuhuma za kukiuka haki za binadamu chini ya utawala war ais Robert Mugabe.

NZ imelitaka Baraza la mchezo wa cricket duniani,kubadili siasa yake inayozitaka timu za cricket kutembelea Zimbabwe kwa mashindano.

Katika mbio za baiskeli za -Tour de France,muamerika George Hincapie,alishinda hatua ya 15 ya masafa ya kilo mita 220.5 hapo jana na hivyo amemtia jeki Lance Amstrong, aliemaliza wapili,kuzidi kupanua mwanya wake kileleni mwa mbio hizo.Lance Amstrong sasa ana kila nafasi ya kunyakua taji lake la 7 la ubingwa wa Tour de France.

Katika mashindano ya ubingwa wa kuogolea ulimwenguni,China imeanza kutamba:China ilinyakua jana medali 2 za dhahabu .Ilikua siku ya ufunguzi wa mashindano hayo mjini Montreal,Kanada.

Na katika ringi ya mabondia,Jermain Taylor alizusha msangao jana alipomvua taji Bernard Hopkins na kuvaa yeye taji hilo la wezani wa wezani wa kati-middle-weight huko Las Vegas.

Hilo lilikua pigo la kwanza kabisa tangu kupita miaka 12 kwa Hopkins.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW