1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Starmer aanza mchakato wa kupunguza makali ya Brexit

2 Oktoba 2024

Waziri Mkuu Keir Starmer wa Uingereza anakwenda Brussels kuanza kutekeleza ahadi yake ya kurejesha upya uhusiano wa nchi yake na Umoja wa Ulaya uliotatizwa na kura ya kujiondowa kwenye Umoja huo, Brexit.

Waziri Mkuu Keir Starmer wa Uingereza
Waziri Mkuu Keir Starmer wa UingerezaPicha: Manuel Balce Ceneta/AP/picture alliance

Starmer atafanya mkutano wake wa kwanza na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von der Leyen, tangu alipoingia madarakani na kukiondoa chama cha Conservative katika uchaguzi mkuu wa mwezi Julai.

Hii ni ishara nyingine ya nia njema ya Uingereza kuelekea kwa majirani zake wa Ulaya, baada ya kujiengua kwenye umoja huo mwaka 2020 chini ya mpango wa Brexit ulioongozwa na aliyekuwa waziri mkuu wa wakati huo, Boris Johnson.

Soma zaidi: Uingereza kutanua ushirikiano katika sekta ya ulinzi na Ujerumani

Mkutano huo unafuatia mikutano ya pande mbili kati yake na Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa, Kansela Olaf Scholz wa Ujerumani na Waziri Mkuu Giorgia Meloni wa Italia.