1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Starmer aonya chama cha Labour UK kinapigania maisha yake

28 Septemba 2025

Chama tawala cha Labour nchini Uingereza kimeanza mkutano wake wa mwaka, huku Waziri Mkuu Keir Starmer akiwashawishi wabunge anaweza kuongoza kile alichokiita “mapambano ya maisha yetu” dhidi ya chama Reform UK.

Waziri Mkuu wa Uingerea Keir Starmer
Waziri Mkuu wa Uingerea Keir Starmer Picha: Leon Neal/Avalon/Photoshot/picture alliance

Starmer, aliyeirejesha Labour madarakani mwaka jana baada ya miaka 14 ya kuwa upinzani, anakabiliwa na tuhuma za kashfa, sera zilizoshindwa na kuporomoka katika kura za maoni. Anasema mpango wa Reform kuhusu wahamiaji ni wa kibaguzi na ungeigawa nchi.

Wachambuzi wanasema uongozi wake uko katika mtihani mkubwa, huku mkutano huu ukihesabiwa kama fursa ya kubadilisha upepo wa kisiasa kabla ya uchaguzi mkuu wa 2029.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW