1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Starmer kuwa mwenyeji wa Zelensky na viongozi wa Ulaya

6 Desemba 2025

Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer, atakutana na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky pamoja na viongozi wa Ufaransa na Ujerumani mjini London Jumatatu, wakati mazungumzo kuhusu kumaliza vita vya Ukraine yanaendelea.

Denmark Copenhagen 2025 | Mkutano wa 7 wa Jumuiya ya Siasa ya Ulaya
Waziri Mkuu wa Albania Edi Rama, Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz, Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky Copenhagen Oktoba 2, 2025Picha: Mads Claus Rasmussen/Ritzau Scanpix/AFP/Getty Images

Starmer atatumia mkutano na Zelensky, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Friedrich Merz kuonyesha uungaji mkono wa Uingereza kwa Ukraine.Watajadili pia mazungumzo yanayoendelea kati ya maafisa wa Marekani na Ukraine yanayolenga kupata makubaliano ya kuhakikisha usalama wa Ukraine baada ya vita.Takribani wiki mbili zilizopita, viongozi hao wanne walishiriki katika mkutano wa mtandaoni wa kile kinachoitwa "muungano wa wenye nia” ulioitishwa na Starmer na Macron ili kutoa kikosi cha kulinda amani cha Ulaya kitakachoweza kupelekwa Ukraine iwapo kutakuwa na usitishaji wa mapigano.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW