1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Starmer kuwasili Poland baada ya ziara yake nchini Ukraine

17 Januari 2025

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer anatarajiwa siku ya Ijumaa kuwasili mjini Warsaw ambapo atakuwa na mazungumzo na Waziri Mkuu wa Poland Donald Tusk.

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer akiwa mjini Kiev
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer akiwa mjini KievPicha: Carl Court/Getty Images

Ofisi ya Starmer ya Downing Street imesema Uingereza na Poland zinatazamiwa kuyajadili makubaliano mapya ya ulinzi na usalama. Starmer amesema Uingereza na Poland ni washirika wa muda mrefu na ushirikiano wao utadumishwa hadi vizazi vijavyo.

Soma pia:Uingereza yaahidi kuihakikishia Ukraine usalama

Haya yanajiri siku moja baada ya Starmer kufanya ziara yake ya kwanza mjini Kiev ambapo kiongozi huyo ameahidi kushirikiana na Ukraine ili kutoa dhamana za kiusalama.

     

     

     

     

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW