1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Starmer: Vigumu kurejesha uhusiano na EU kama awali

3 Oktoba 2024

Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer amekiri kwamba haitokuwa rahisi kuyarejesha tena mahusiano mazuri ya nchi yake na Umoja wa Ulaya.

Brussel, Ubelgiji | Keir Starmer na Ursula von der Leyen.
Waziri Mkuu wa Uingereza Keir Starmer akiwa na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen.Picha: Benjamin Cremel/AP/picture alliance

Starmer ameyasema haya licha ya hali iliyoboreka kidogo kati ya pande hizo mbili baada ya hatua ya Uingereza kujiondoa kutoka kwenye Umoja wa Ulaya, Brexit.

Starmer amefanya mazungumzo na Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya Ursula von der Leyen, wakati ambapo serikali yake ya Labour inatafuta mwanzo mpya na umoja huo ulio na wanachama 27 baada ya kuwashinda Wahafidhina katika uchaguzi wa mwezi Julai. 

Soma pia:Umoja wa Ulaya waikaribisha Uingereza kwa mashirikiano

Viongozi hao wawili wamekubaliana kufanya mikutano ya mara kwa mara ya kilele huku wa kwanza ukiratibiwa kufanyika katika nusu ya kwanza ya mwaka ujao, huku wakitafuta maeneo ambayo wanaweza kushirikiana.

 Kwa upande wake Von der Leyen ambaye alikutana na Starmer pia katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwezi uliopita, amesema misukosuko inayoikumba dunia kwa sasa inaonesha umuhimu wa majirani hao kushirikiana. 
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW