1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Steinmeier aanza ziara ya siku 3 Uhispania

26 Novemba 2025

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier anaanza ziara ya siku tatu nchini Uhispania Jumatano.

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier na mkewe Elke wakiwa na Mfalme Felipe VI wa Uhispania na mkewe Malkia Letizia
Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier na mkewe Elke (kushoto) wakiwa na Mfalme Felipe VI wa Uhispania na mkewe Malkia Letizia (kulia)Picha: Lisi Niesner/REUTERS

Steinmeier na mkewe Elke Büdenbender wamekaribishwa mjini Madrid na Mfalme Felipe VI na Malkia Letizia, ambao pia wataandaa chakula cha jioni kwa ajili ya wageni wao baadae Jumatano.

Wafalme hao wa Uhispania walifanya ziara ya kitaifa nchini Ujerumani Oktoba 2022. Kulingana na afisi ya Steinmeier, ziara hiyo Inatarajiwa kuangazia uhusiano mzuri wa mataifa mawili ya Uhispania na Ujerumani.

Rais Steinmeier na Mfalme FelipePicha: Getty Images/AFP/J. Soriano

Ziara hiyo inalenga pia kuonesha mshikamano baina ya mataifahayo ambayo ni washirika wanaounga mkono Umoja wa Ulaya.

Suala jengine litakalokuwa kwenye ajenda ya viongozi hao ni ushirikiano wa kiuchumi, kwani Mfalme Felipe Vi na Steinmeier wanapanga kufungua mkutano wa kiuchumi wa Ujerumani na Uhispania kwa pamoja hapo Alhamis.

Steinmeier pia anapanga kukutana na Waziri Mkuu Pedro Sanchez huku mazungumzo yao yakitarajiwa kujikita katika vita vya Urusi nchini Ukraine.

Hivi majuzi Uhispania ilitoa ahadi ya msaada wa yuro milioni 817 kwa Ukraine.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW