1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Steinmeier afanya mazungumzo na Mwanamfalme wa Saudia

4 Februari 2025

Rais wa Ujerumani frank-Walter Steinmeier amekutana na Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman mjini Riyadh, wakati akianza ziara yake ya siku tatu katika eneo la Mashariki ya Kati.

Steinmeier na Salman
Rais wa Ujerumani frank-Walter Steinmeier akiwa na mwenzake Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed bin Salman mjini Riyadh.Picha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Steinmeier amekaribishwa kwa heshima kijeshi kabla kufanya mazungumzo yaliyojikita katika mustakabali wa Syria baada ya kuanguka kwa utawala wa Bashar al-Assad na hali ya Gaza kufuatia usitishwaji mapigano kati ya Israel na wanamgambo wa Hamas.

Ujerumani na Saudi Arabia yote yanapendelea suluhu la mataifa mawili kati ya Waisraeli na Wapalestina.

Mengine yaliyojadiliwa na viongozi hao wawili ni utawala mpya wa Marekani chini ya Rais Donald Trump pamoja na ushawishi wa Iran. Steinmeier ndiye rais wa kwanza wa Ujerumani kufanya ziara nchini Saudi Arabia.

Steinmeier akutana na Mohammed bin Salman mjini Riyadh

Rais huyo wa Ujerumani ataizuru Jordan ambapo atakutana na wanajeshi wa Ujerumani katika kambi ya al-Azraq lakini pia atakutana na Mfalme wa Jordan Abdullah wa pili.

Atakamilisha ziara yake Jumatano atakapokutana na Rais wa Uturuki Reccep Tayyip Erdogan kuijadili hali ya Syria.   
 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW