1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Steinmeier: Hali Mashariki ya Kati bado ni ya wasiwasi

2 Novemba 2025

Steinmeier amesema watu katika eneo hilo wana matumaini kwamba mchakato wa amani katika Ukanda wa Gaza utaendelea baada ya usitishaji mapigano kati ya Israel na Hamas ingawa wengi wao wana hofu juu ya ugumu uliopo.

 2025 |Steinmeier I t Nawaf Salam
Rais wa Ujerumani Frank Walter Steinmeier na Waziri Mkuu wa Lebanon Nawaf SalamPicha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ameelezea wasiwasi wake kuhusu hali huko Mashariki ya Kati baada ya kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Lebanon Nawaf Salam na Rais wa Misri Abdel-Fattah al-Sissi mjini Cairo hii leo.

Steinmeier amesema watu katika eneo hilo wana matumaini kwamba mchakato wa amani katika Ukanda wa Gaza utaendelea baada ya makubaliano ya usitishaji mapigano kati yaIsrael na Hamasingawa wengi wao wana hofu juu ya ugumu uliopo mbele yao.

Rais wa Ujerumani yuko katika ziara ya karibu wiki moja barani Afrika. Aliwasili Misri hapo jana ambapo alihudhuria pia ufunguzi rasmi wa Jumba la Makumbusho la Grand Egyptian mjini Cairo.

Ofisi yake imesema baada ya Misri, kiongozi huyo ataelekea katika mataifa ya Ghana na Angola ambapo analenga kutambua jitihada za amani na utulivu za mataifa hayo mawili katika ukanda wa Afrika Magharibi.