Itikadi kali za mrengo zinatishia demokrasia Ujerumani
9 Novemba 2025
Matangazo
Steinmeier amezungumzia kuhusu ongezeko la siasa kali za mrengo wa kulia katika mfumo wa chama kinachopinga wahamiaji cha Alternative for Germany (AfD), ambacho kilipata asilimia 20.5 ya kura katika uchaguzi mkuu wa Februari na kushika nafasi ya pili.
Ujerumani yaadhimisha miaka 36 tangu kuanguka ukuta wa Berlin
Rais Steinmeier ametoa kauli hiyo katika makazi yake rasmi mjini Berlin wakati Ujerumani inaadhimisha leo miaka 36 tangu kuanguka kwa Ukuta wa Berlin. Tukio hilo lilihitimisha enzi ya utengano na kufungua njia ya kuungana tena kwa iliyokuwa Ujerumani Magharibi na Mashariki.