1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Steinmeier: Sote tunamani ulimwengu wa amani zaidi

25 Desemba 2023

Rais wa Ujerumani Frank-Walter Steinmeier ameelezea haja ya ujasiri na ushirikiano katika kukabiliana na changamoto nchini Ujerumani na duniani kote.

Ujerumani| Hotuba ya Krismas ya Rais wa Shirikisho Steinmeier
Rais wa Shirikisho la Ujerumani Frank-Walter Steinmeier amewataka Wajerumani kushirikiana kulinda demokrasia.Picha: Britta Pedersen/dpa/picture alliance

Katika hotuba yake ya kila mwaka ya Krismasi aliyoitoa usiku wa kuamkia leo, Steinmeier amesema, mwaka huu, kwa hakika ulimwengu umedhihirisha upande wake wa giza.

Ameongeza kuwa vita vya uchokozi vya Urusi dhidi ya Ukraine sasa vinaingia katika msimu wa pili wa majira ya baridi kali.

Steinmeier amezungumzia pia yanayojiri Mashariki ya Kati ukiwemo ule aliouita "ukatili wa Hamas" na yanayotokea kwa wahanga wa vita vya eneo hilo.

Soma pia: Steinmeier awaonya wananchi kutoipa kisogo demokrasia

Licha ya changamoto hizo, Steinmeier amesisitiza umuhimu wa matumaini na haja ya kuukaribia mwaka mpya kwa ujasiri.

Rais huyo wa Ujerumani amesisitiza umuhimu wa kudumisha demokrasia imara, akisema hilo linaweza kutokea tu ikiwa watu watashirikishwa na ikiwa watajitahidi kuhakikisha kwamba kile ambacho bado hakijawa kizuri leo, kinakuwa bora kesho.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW