Migogoro
Mwakilishi wa Marekani kukutana na Vladimir Putin Urusi
26 Novemba 2025
Matangazo
Mazungumzo hayo yanatarajiwa kufanyika wakati Marekani ikiendelea kushinikiza mazungumzo ya usuluhishi kwa ajili ya mpango wa kuumaliza mzozo wa Ukraine. Kremlin imeongeza kuwa, sehemu ya mpango wa sasa wa Marekani zinaleta matumaini, lakini bado kuna vipengele vinavyohitaji mjadala.
EU yasisitiza iko bega kwa bega na Ukraine
Wakati huo huo, Rais wa Halmashauri Kuu ya Umoja wa Ulaya, Ursula von Der Leyen amesema chombo chake kipo tayari kuwasilisha nyaraka za kisheria kuhusu matumizi ya mali za Urusi zinazoshikiliwa kutokana na vita vya Ukraine.
Ameyasema hayo katika hotuba yake mbele ya Bunge la Ulaya na kuongeza kuwa Umoja wa Ulaya unaiunga mkono Ukraine katika kila hatua hadi amani itakapopatikana. Von der Leyen amepongeza pia juhudi zinazofanywa na Marekani kuutatua mzozo huo.