STIKO yapendekeza chanjo kwa watoto wa zaidi ya miaka 12
14 Januari 2022Matangazo
Waziri wa Afya wa Ujerumani, Karl Lauterbach tayari ameshawaambia wazazi wapange kuwapatia watoto wao chanjo ya nyongeza na wasisubiri hadi litakapotolewa tamko rasmi.
Kwa mujibu wa taasisi ya kudhibiti magonjwa ya kuambukiza Ujerumani, Robert Koch watoto hao watapewa chanjo kulingana na umri wao, miezi mitatu au zaidi baada ya kupata chanjo ya mwisho.
Pendekezo hilo pia linasema kwamba kundi hilo linapaswa kupewa tu chanjo ya BioNTech-Pfizer.
Wakati huo huo, uongozi wa uwanja wa ndege wa Hong Kong umesema leo kuwa abiria kutoka zaidi ya nchi 150 duniani watazuiwa kupita kwenye uwanja huo, ikiwa ni hatua ya kukabiliana na kuenea kwa virusi vya corona.