1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Stockholm.Nchi wahisani kujadili kuisaidia Lebanon kibiashara.

31 Agosti 2006

Wawakilishi wa zaidi ya nchi 60 na mashirika ya kimataifa hivi sasa wanakutana pamoja mjini Stockholm katika mkutano wa wachangiaji wenye nia ya kuisaidia Lebanon.

Maafisa nchini Sweeden ambayo ndio wenyeji wa mkutano huo wamesema wanatazamia kukusanya kiasi cha dola milioni mia tano kwa ajili ya kuisaidia Lebanon.

Umoja wa Ulaya tayari umeshaahidi kutoa Euro milioni 42 kama msaada wake.

Kamishna wa masuala ya nje wa Umoja wa Ulaya Benita Ferrero-Waldner amewaambia waandishi wa habari mjini Brussels kuwa idadi hiyo kubwa ya msaada ni kwa lengo la kuisaidia Lebanon kibiashara.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW