Stoltenberg asema anataraji msaada wa kutosha kwa Ukraine
10 Julai 2024Stoltenberg alikuwa akizungumza na waandishi habari muda mfupi kabla ya kuanza kwa mkutano wa kilele wa Jumuiya ya NATO unaofanyika mjini Washington ambao kwa mara nyingine unakubikwa na kiwingu cha vita vya Ukraine.
"Tutafanya pia maamuzi muhimu kwa ajili ya siku zijazo: kuhusu yale yanayoendelea Ukraine na jinsi ya kutanua maingiliano yetu hususani na washirika wetu wa kanda ya Asia na Pasifiki. Kuhusu Ukraine, ninataji washirika watakubaliana kiwango cha msaada wa kukidhi mahitaji".
Soma pia:Viongozi wa NATO kutangaza msaada kwa Ukraine
Katika hatua nyingine Waziri wa mambo ya kigeni wa Marekani Antony Blinken ametangaza kuwa washirika wa NATO tayari wameanza kuipelekea Ukraine, ndege mamboleo za kivita chapa F-16 kuisaidia kuimarisha ulinzi wake wa anga.
Amesema ndege kutoka Denmark na Uholanzi ziko njiani kwenda Ukraine.