1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaUkraine

Stoltenberg: NATO inatakiwa kujiimraisha kisilaha, 2023

2 Januari 2023

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami NATO Jens Stoltenberg amesema katika mahojiano jana kuwa jumuiya hiyo inafaa kuongeza uzalishaji wa silaha.

Rumänien Bukarest | Treffen der NATO-Außenminister | Jens Stoltenberg, NATO-Generalsekretär
Picha: Andrei Pungovschi/AFP/Getty Images

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami NATO Jens Stoltenberg amesema hayo katika wakati ambapo vita vya nchini Ukraine bado vinaendelea.

Ameliambia shirika la habari la Uingereza BBC kuwa, wanahitaji silaha kwa wingi.

Katibu Mkuu huyo wa NATO ameeleza kuwa matengenezo ya mifumo ya silaha ambayo tayari imewasilishwa nchini Ukraine ni muhimu kama ulivyo mjadala wa kuisambazia Kiev silaha zaidi.

Stoltenberg amesema kwamba dalili zote zinaonyesha kuwa Urusi haijakata tamaa na nia yao ya kuchukua udhibiti kamili wa Ukraine na kuwa Moscow iko tayari kuendelea na vita.