1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW
SiasaMarekani

Stoltenberg: NATO kufanya maamuzi muhimu kuhusu Ukraine

18 Juni 2024

Jumuiya ya NATO yaangazia kufanya maamuzi muhimu kuhusu Ukraine katika mkutano wa kilele mwezi Julai.

Rais wa Marekani Biden akutana na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya NATO Jens Stoltenberg
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya kujihami ya NATO Jens Stoltenberg akikutana na rais wa Marekani Joe Biden katika ikulu ya White House marekaniPicha: Mark Schiefelbein/AP/dpa/picture alliance

Rais wa Marekani Joe Biden amefanya mazungumzo na Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Kujihami, NATO Jens Stoltenberg siku ya Jumatatu.

Baada ya mkutano huo, Stoletenberg aliwaambia waandishi wa habari kwamba, alikuwa na mazungumzo mazuri na Biden na walijadiliana juu ya mkutano ujao wa kilele wa NATO mjini Washington DC, mnamo mwezi Julai.

"Tulijadiliana juu ya mkutano ujao wa kilele wa NATO hapa Washington mwezi ujao, ambapo tutakuwa tunasherehekea miaka 75 ya mafanikio makubwa katika historia ya muungano huu, lakini pia ni mahali ambapo huwa tunafanya maamuzi muhimu kwa ajili ya siku za usoni na hasa matumizi ya ulinzi. Lakini pia tutafanya maamuzi muhimu juu ya Ukraine," amesema Jens Stoltenberg.

Stoltenberg aidha ametangaza kwamba zaidi ya washirika 20 wa NATO watatumia asilimia 2 ya pato jumla la ndani katika bajeti ya ulinzi kwa mwaka huu.