STRASBOURG: Pöttering achaguliwa rais wa Bunge la Ulaya
17 Januari 2007Matangazo
Mwanasiasa wa Kijerumani wa chama cha Christian Demokrats,Hans-Gert Pöttering,amechaguliwa rais wa Bunge la Ulaya,mjini Strasbourg.Tangu mwanzoni,ilijulikana kuwa atachaguliwa,baada ya chama chake cha „Umma wa Ulaya“ kuafikiana na chama cha Wasoshalisti bungeni,kugawana awamu ya miaka mitano.Mhispania,Josip Borrell wa chama cha kisoshalisti alichaguliwa rais wa bunge mwaka 2004,lakini amejiuzulu baada ya kushika wadhifa huo kwa nusu ya kipindi chake,ili kumpisha Pöttering alie na umri wa miaka 61 kuendelea na sehemu ya pili ya awamu.