1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

STRASBOURG-Taratibu za utoaji viza kwa wageni nchini Ujerumani hazikuwa zinaendana na sheria za Umoja wa Ulaya.

11 Mei 2005

Afisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya mjini Strasbourg,amesema taratibu za zamani za Ujerumani za kuwapatia viza wageni,hazikuwa zinaendanana na sheria za Umoja wa Ulaya.

Waziri wa Sheria wa Umoja wa Ulaya ambaye pia anasimamia Tume ya Mambo ya Ndani,Franco Frattini,amesema taratibu zilizokuwepo katika ubalozi mdogo wa Ujerumani nchini Ukraine kati ya mwaka 2000 na mwaka 2002,hazikuwa katika mpangilio.

Ameongeza kusema kuwa taratibu za Ujerumani hazikutoa nafasi ya ukaguzi wa kina kwa waombaji wa viza juu ya afya zao na pia kuwepo nia kwa mwombaji kutaka kurejea nchi anayotoka.

Mwezi uliopita,Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Joschka Fischer,alikubali kubeba jukumu la sera za nchi,kuhusiana na masuala ya viza kwa kipindi hicho.

Upande wa upinzani nchini Ujerumani umedai kuwa sera hizo zilitoa mwanya kwa wahalifu kuweza kuingia nchini.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW