1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Strasbourg.Bulgaria na Romania zakubaliwa kujiunga na Umoja wa Ulaya.

26 Septemba 2006

Kamisheni kuu ya Umoja wa Ulaya imeziruhusu Bulgaria na Romania zijiunge na Umoja wa Ulaya kuanzia January mosi mwakani lakini kamisheni kuu imetaka nchi hizo mbili ziwe chini ya ukaguzi mkali wa Umoja huo.

Mwenyekiti wa kamisheni kuu ya Umjoa wa Ulaya Jose Manuel Durao Barroso ametangaza hayo mbele ya wabunge wa Ulaya mjini Strasbourg.

Chanzo cha masharti hayo kimetokana na mageuzi haba yaliyofanywa na nchi hizo katika kupambana na visa vya uhalifu na rushwa.

Bulgaria na Romania zitakuwa ni kati ya nchi masikini kabisa katika wanachama wa Umoja wa Ulaya; Aidha kuingia kwao katika umoja huo unafanya Umoja wa Ulaya kuwa na wanachama 27 kwa sasa.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW