Stuttgart na Hertha Berlin, nani ataponea mechi ya mchujo?
9 Mei 2022Matangazo
Nafasi iliyosalia ni ya 16 ambayo inashikiliwa na VfB Stuttgart kwa sasa wakiwa na pointi 30 na juu yao katika nafasi ya 15 wapo Hertha BSC Berlin wenye pointi 33.
Timu zote hizi zinasubiri mechi zao za mwisho kuamua iwapo zitasalia katika Bundesliga moja kwa moja au zicheze mechi ya mchujo itakayoamua iwapo zitasalia au kushuka daraja.
Kwa kawaida timu inayomaliza ligi kwenye nafasi ya 16 ndiyo inayocheza mechi hiyo na timu iliyomaliza ya tatu kwenye ligi ya daraja la pilina mshindi anacheza Bundesliga msimu unaofuata.
Katika mechi ya mwisho VfB Stuttgart watakuwa wenyeji wa FC Köln kisha Hertha BSC Berlin wawatembelee Borussia Dortmund uwanjani Signal Iduna Park.