1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Stuttgart waangukia pua mikononi mwa Fenerbahce ya Uturuki

24 Oktoba 2025

Timu inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani Bundesliga, VfB Stuttgart imelazwa 1-0 na Fenerbahce ya Uturuki usiku wa kuamkia leo katika mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Ulaya.

Mchezaji wa Stuttgart Jamie Leweling
Mchezaji wa Stuttgart Jamie LewelingPicha: Ralf Brueck/Jan Huebner/IMAGO

Bao la Fenerbahce lilifungwa na Kerem Aktürkoglu kupitia mkwaju wa penalti katika dakika ya 34 ya mechi, baada ya Angelo Stiller kumuangusha Milan Skriniar. Hii ni mechi ya pili mfululizo Stuttgart kufungwa katika mashindano hayo.

Kocha wa stuttgart Sebastian Hoeness amesema wanatoka huko Uturuki wakiwa wanajivunia kwa mchezo mzuri walioucheza kwani ndivyo walivyopanga kucheza licha ya kuwa hakuweza kupata pointi tatu muhimu.

Fenerbahce ambao wanafunzwa na kocha raia wa Ujerumani Domenico Tedesco, kwa sasa wana jumla ya pointi sita baada ya kupata ushindi katika mechi yao iliyopita walipochuana na Dinamo Zagreb.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW