1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

STUTTGART: Wakimbizi kutoka Kosovo na Afghanistan warejee nyumbani

25 Juni 2005

Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani,Otto Schilly na mawaziri wenzake kutoka majimbo 16 ya Ujerumani wamekubali kuwa wakimbizi waliokuja Ujerumani wakati wa migogoro ya Kosovo na Afghanistan,sasa wanapaswa kurejea nyumbani.Hayo yalikubaliwa katika mkutano uliofanywa mjini Stuttgart,kusini mwa Ujerumani.Baada ya mkutano huo,waziri wa ndani wa jimbo la Baden-Württemberg,Heribert Rech,aliwaambia maripota kuwa wakimbizi wanaweza kurejea nyumbani kwa sababu katika nchi hizo mbili,sasa kuna usalama wa kutosha.Akasema kwamba ni matumainio yao kuwa wakimbizi watarejea makwao kwa hiyari.Kwa wakati huo huo aliongezea kuwa wakimbizi walio wakapera huenda wakafukuzwa kurejea Kosovo na Afghanistan.Mawaziri hao vile vile wamekubali kuwa na sheria kali kuhusu wahamiaji wa Kiyahudi kutoka Ulaya ya mashariki.Sasa wahamiaji hao watahitaji kuonyeysha kuwa wanafahamu msingi wa lugha ya Kijerumani na pia wawe na ushahidi kwamba wanaifuata dini ya Kiyahudi.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW