1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Stuttgart yaibamiza Celtic katika Ligi ya Ulaya

20 Februari 2026

Michezoni klabu inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani, Bundesliga, VfB Stuttgart imepata ushindi wa 4-1 dhidi ya miamba wa Scotland Celtic katika mechi ya Ligi ya Ulaya iliyochezwa usiku wa kuamkia leo, huko Glasow.

Winga wa Stuttgart Jamie Leweling
Winga wa Stuttgart Jamie LewelingPicha: Ralf Brueck/Jan Huebner/IMAGO

Bilal El Khannouss aliwafungia Stuttgartmabao mawili kisha Jamie Leweling na Tiago Tomas wakafunga mabao mengine ya Stuttgart.

Celtic walipewa bao la kufutia jasho na BenjaminNygren na kushindwa huko kwa mabao 4 kulimaanisha kuwa kocha wao mpya Martin ONeill amerudi katika klabu hiyo kwa mguu mbaya, kwani ilikuwa mechi yake ya kwanza kama kocha mpya.

Kwengineko Viktoria Plzen wamesalia kuwa timu ya pekeekatika mashindnao hayo kutopoteza mechi kufikia sasa baada ya sare yao ya 2-2 na Panathinaikos ya Ugiriki.

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW