Sudan iko tayari kushirikiana na Marekani na Saudia
20 Novemba 2025
Katika taarifa yake, baraza hilo limeishuruku Marekani na Saudi Arabia kwa juhudi zao zinazoendelea za kuzuia umwagaji wa damu Sudan.
Aidha, limeelezea utayari wake wa kushirikiana nao kwa dhati ili kupata amani ambayo watu wa Sudan wanaitarajia.
Kauli hiyo imetolewa baada ya Rais wa Marekani, Donald Trump kusema kuwa atashirikiana na Saudi Arabia, Umoja wa Falme za Kiarabu na Misri, kuumaliza mzozo kati ya jeshi la Sudan na wanamgambo wa RSF.
Trump azungumzia ukatili wa Sudan
''Ukatili mkubwa unafanyika Sudan. Pamekuwa mahali penye vurugu zaidi duniani. Chakula madaktari na kila kitu kingine vinahitajika sana,'' alifafanua Trump.
Kulingana na Trump, viongozi wa nchi za Kiarabu kutoka ulimwenguni kote, wamemuomba atumie mamlaka na ushawishi wa urais kusimamisha mara moja kile kinachoendelea Sudan.
Wakati wa ziara yake mjini Washington, Mwanamfalme wa Saudia, Mohammad bin Salman, alimuomba Rais Trump kusaidia kuleta amani katika taifa hilo la Afrika.