1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan: Jeshi lashindwa kuwaondoa waandamanaji

Zainab Aziz Mhariri:Yusuf Saumu
15 Aprili 2019

Waandamanaji wa Sudan bado wamekaa nje ya makao makuu ya jeshi katika jiji la Khartoum baada ya kufaulu kulizuia jeshi kuusambaratisha mkusanyiko wao katika harakati za kuendeleza maaandamnao yao.

Sudan Proteste in Khartum
Picha: Reuters

Waandamanaji hao wamesimama imara dhidi ya hatua ya jeshi lillojaribu kuondoa vizuizi walivyovuiweka waandamanaji hao, kwa mujibu wa watu walishuhudia wamesema mwishowe wanajeshi walishindwa. Baraza la  mpito la kijeshi, lililochukua mamlaka tangu siku ya  Alhamisi limeahidi kukabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia katika muda wa miaka miwili ijayo.

Hata hivyo baadhi ya makundi yanayoshiriki kwenye maandamano hayo yanalitaka baraza la kijeshi likabidhi mamlaka kwa raia baada ya baraza hilo kumng'oa madarakani rais Omar al-Bashir. Makundi hayo yamegoma kuondoka mabarabarani. Wakati huo huo, kuna ripoti kwamba wanachama wa chama cha kiongozi aliyoondolewa madrakani Omar al Bashir cha National Congress Party (NCP) wameanza kukamatwa.

Msemaji wa baraza la kijeshi Luteni Jenerali Shamseldin Kibashi, amesema wanachama wa chama cha NCP hawaruhusiwi kushiriki katika mazungumzo juu ya serikali mpito wala hakitaruhusiwa kujiunga na serikali ya mpito ya kiraia na kwamba kiongozi wa kiraia atachaguliwa na vyama vya upinzani.

Rais wa Sudan aliyeondolewa madarakani Omar al- BashirPicha: Getty Images/AFP/A. Shazly

Msemaji huyo  pia amewataka wapinzani waungane na kumteua waziri mkuu. Omar al- Bashir mwenyewe alikamatwa siku ya Alhamisi, baada ya jeshi kumtelekeza kwa miezi kadhaa iliyokumbwa na  maandamano ya kuipinga serikali yake.

Jumatatu,balozi wa Uingereza nchini Sudan, Irfan Siddiq, alisema alikutana na naibu mkuu wa baraza la  kijeshi na aliomba kupewa taarifa juu ya mahali alipo Omar al Bashir. Balozi Siddiq pia ametaka iundwa haraka serikali ya mpito ya kiraia kupitia mchakato wa uwazi, wa kuaminika na wa kuzijumuisha pande zote.

Watawala wa kijeshi wa Sudan wanakabiliwa na shinikizo kutoka kwa waandamanaji na serikali za Magharibi. Marekani, Uingereza na Norway zimelitaka baraza la kijeshi la Sudan lifanye mazungumzo na pande zote juu ya kutayarisha kipindi cha mpito kuelekea kwenye utawala wa kiraia. Mabalozi wa nchi hizo wameonya dhidi ya matumizi ya nguvu kwa lengo la kuuzima upinzani wa wananchi. Nchi hizo  zimesema madai halali ya watu wa Sudan bado hayajatekelezwa.

Vyanzo:/DPA/AFP

 

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW