Sudan klushirikiana na FBI
5 Januari 2008Matangazo
KHARTOUM:
Wakuu nchini Sudan wameahidi kushirikiana na timu ya majasusi 4 wa shirika la upelelezi la Marekani FBI kuchunguza kisa cha kupigwa risasi na kuuwawa kwa mjumbe wa kibalozi wa marekani nchini Sudan.
Wizara ya nje ya Marekani imearifu huenda ikapeleka Sudan wachunguzi zaidi kuchunguza kuuwawa kwa John Granville,alietumikia shirika la maendeleo la Marekani USAID.Kikundi cha waislamu wenye itikadi kali kimejitwika dhamana ya mauaji yake.