1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sudan kusini yaondoa kikwazo kwa serikali ya Umoja wa Taifa

Sekione Kitojo
15 Februari 2020

Viongozi hasimu wa Sudan kusini wameondoa kiunzi kikubwa ikiwa imebaki wiki moja tu kabla ya muda wa mwisho wa kuunda serikali ya Umoja wa Iitaifa, ambapo rais alitangaza"muafaka wa maumivu".

Uganda Friedensgespräche in Entebbe
Picha: Presidential Press Unit of Uganda

Kikwazo hicho kilichokuwa  kinazuwia  uundwaji  wa  serikali  ya  Umoja  wa  Kitaifa  ni  suala  nyeti kisiasa juu ya idadi ya majimbo.

Rais Salva Kiir  amesema  baada  ya  mkutano na  hasimu  wake Riek Machar jana Ijumaa (14.02.2020) ameamua  kuirejesha  nchi hiyo  changa  duniani kuwa  na  majimbo 10 pamoja  na  maeneo matatu  ya  utawala, na  kupunguza suala "kuu la mvutano" wakati nchi hiyo  ikijitoa  kutoka  katika  vita  vya  wenyewe  kwa  wenyewe.

Rais wa Sudan kusini Salva KiirPicha: Reuters/S. Bol

Makubaliano hayo yatasaidia  kuipeleka  nchi  hiyo kuvuka "mzozo huu usiokuwa na sababu", rais  amesema, akiuita  muafaka  huo kuwa  ni "moja  katika  maamuzi magumu yanayoumiza ambayo hajawahi  kuyafanya."

Mbinyo  wa  kimataifa  kutoka  Marekani  na  mataifa  mengine umekuwa  ukiongezeka  dhidi  ya  Kiir  na  Machar  kufikia  muda  wa mwisho  wa  Februari 22 kujiunga  pamoja  katika  serikali  ya  Umoja wa  Kitaifa. Muda  huo  wa  mwisho  umerefushwa  mara  mbili katika  mwaka  mmoja  uliopita. Machar atarejea  kama  makamu  wa rais  wa  Kiir, jukumu  ambalo  mara  mbili zilisababisha   mzozo.

Marekani, ambayo ni mfadhili  mkuu wa  misaada  ya  kiutu  nchini Sudan kusini, ilichukua  hatua  muhimu katika  wiki  za  hivi  karibuni za  kuweka  vikwazo  kwa  makamu wa  kwanza  wa  rais  wa  Kiir, Taban Deng Gai.

Makamu wa kwanza wa rais wa Sudan kusini Taban Deng GaiPicha: Getty Images/AFP/S. Bol

Utaratibu wa  usalama bado ni suala gumu

Masuala  magumu bado  yanaendelea  kuwapo, ikiwa  ni  pamoja  na utaratibu  wa  usalama ambao  ni  pamoja  na  kuunganisha  maelfu ya  wanajeshi  wa  zamani  waliokuwa  wakipigana kuwa jesho  moja la  taifa.

Mchakato  huo  umeshuhudia  uchelewesho  mara  kadhaa.

Makamu wa rais wa zamani wa Sudan Kusini Riek MacharPicha: Reuters/S. Bol

Vita  vya  wenyewe kwa  wenyewe  vya  miaka  mitano, ambavyo vilizuka miaka miwili tu kufuatia  uhuru wa  nchi  hiyo  kutoka  Sudan, vimeuwa  watu 400,000 na  mamilioni  kukimbia  makaazi  yao.

Uchumi  wa  nchi  hiyo  umevurugika na  karibu nusu  ya  nchi  hiyo imekuwa  katika  mzozo  mkubwa  wa  njaa  kali.

Idadi  ya  majimbo  limekuwa  suala  la  kubishaniwa na  kuleta mivutano  kwa  miaka  kadhaa. Makubaliano ya  amani  ya  mwaka 2015 yaliyoshindwa  yaliongeza  idadi ya  majimbo  kutoka  10  hadi 32. Hadi sasa, serikali  imesisitiza kuwa na  idadi  hiyo, wakati upinzani  unaoongozwa  na  Machar ulitaka  mbadala wa majimbo 23 ama  10.

Kuna nafasi kubwa ya kumaliza mzozo wa vita iwapo serikali mpya ya Umoja wa Kitaifa itaundwaPicha: picture-alliance/Photoshot/Xinhua/G. Julius

Wiki moja  iliyopita, wakati viongozi  wa  kanda  wakiweka  mbinyo mpya, Kiir aliomba  kuongezewa  muda  zaidi kupata  ushauri  kwa watu  nyumbani  kuhusu  suala  hilo. Maelezo ya  tangazo  la Jumamosi sasa  yatapelekwa  kwa  viongozi wa   bodi ya  kanda  ya Afrika  mashariki  pamoja  na  upande  wa  Machar.

 

Ruka sehemu inayofuata Taarifa kuu ya DW

Taarifa kuu ya DW

Ruka sehemu inayofuata Taarifa zaidi kutoka DW