Sudan Kusini yasitisha mpango wa kubadilisha sarafu
16 Oktoba 2020Kama anavyoeleza mwandishi wetu wa mjini Juba Omar Mutasa, mpango wa kubadilisha sarafu hiyo sasa umesimamishwa.
Waziri wa habari MICHEAL MAKUEI akiwa pia msemaji wa serikali ya Sudan Kusini alisema serikali itaweka pesa za dollar kwenye hazina ya Benki kuu ya taifa na pia kwenye Benki za kibiashara kusaidia kupunguza mfumko wa bei.
Bunge la Sudan Kusini limeidhinisha mkopo wa Dola milion 250 kutoka Benki ya Exim ili kunusuru uchumi wa nchi usizidi kuporomoka.
Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya kiuchumi wanasema mkopo utasaidia kuleta suluhisho la muda mfupi tu, na sio la kudumu, kama alivyonieleza DENG MAKUR mhadhiri na mkuu wa kitengo cha uchumi wa chuo kikuu cha Juba. "HATA IKIWA SERIKALI INA PESA ,HIO ITAKUA SULUHU YA MUDA TU, SIO SULUHU YA KUDUMU,HATUAMINI KATIKA SULUHU YA MUDA TU."
Makur Amefafanua suluhu ya kudumu serikali ya umoja wa kitaifa ya Sudan Kusini inayofa kuzingatia. "IKIWA KUNA UTULIVU WA KISIASA ,UTULIVU WA KIUSALAMA ,SERIKALI LAZIMA IPIGE VITA RUSHWA NA UFISADI, KUTOKUWEKO UWAZI IMESABABISHA RUSHWA KUKITHIRI SANA SUDAN KUSINI IKIWA NI YAPILI KWA RUSHWA DUNIANI BAADA YA SOMALIA."
Wananchi wa kawaida nao wametoa maoni yao kuhusiana na hali hii ya kuzidi kupanda kwa gharama ya maisha.
Wakati huohuo Prof Joram Biswaro Balozi wa Umoja wa Afrika hapa Sudan Kusini amezungumza na rais Salva Kiir Meyardit kuhusu suala hilo la kubadilisha sarafu mpya ya Sudan Kusini
Tangazo la kubadilisha sarafu ya pound ya Sudan Kusini lilitangazwa Jumapili iliopita na waziri MICHEAL MAKUEI msemaji mkuu wa serikali ya Sudan Kusini.
Juma tano wiki hii wafanya biashara walifunga maduka yao wakihofia kupata hasara Dola moja ilipofikia pound za Sudan Kusini 750 katika soko mitaani badala ya bei rasmi ya serikali ya pound za Sudan Kusini 165 kwa dola moja.
Mwandishi: Omar Mutasa/DW Juba